Pages - Menu

Pages

Sunday, 14 July 2013

Muhogo wa nazi wa ngisi


Mahitaji
Mfuko mmoja wa mihogo
Ngisi nusu kilo
Nazi kopo moja
chumvi kijiko kimoja cha chai

Jinsi ya kupika
kata kata mihogo yako ioshe weka katika sufuria weka chumvi ichemshe hadi iive.
chukua ngisi wako waweke katika sufuria wachemshe kidogo bila ya kuweka maji maana watajitoa maji wenyewe sababu umewaosha,baada ya kuwachemsha kidogo mimina ngisi na yale maji yake katika mihogo chemsha tena kidogo mimina nazi yako wacha ichemke hadi tui liive.
Epua tayari kwa kuliwa.  

No comments:

Post a Comment