Saturday, 18 April 2015


Glamour World and Food Section..... Get best of your day from Primacla 

Decorations & Catering. 
Get a different best day look by decorating with PRIMACLA and make your day perfectly great in your wedding,birthdays,sendoff, anniversary,kitchen party,baptism and even in funeral ceremony.  




In Decor and catering Primacla treats you peculiar. Contact: +255754710600, +255659468484, +2557672444000, email: fnkya57@gmail.com
Insta: faithnkyaberege


Sunday, 22 February 2015



Wednesday, 5 November 2014


Mahitaji 

Ngisi kiasi

Chumvi nusu kijiko cha chai

Pilipili mtama 1/2 kijiko cha chai

Nyanya fresh moja 

Ndimu/limao nusu kipande

Pilipili hoho 1/2kwa kila rangi

Maji ya mag mbili 


Jinsi ya kupika safisha ngisi wako vizuri weka katika sufuria bandika jikoni weka Chumvi na pilipili mtama wacha ngisi watajitoa maji yakikauka weka maji na ndimu,pilipili hoho na Nyanya fresh moja wacha vichemke kwa dk kumi epua supu yako tayari .

Unaweza kula kwa mkate,chapati


    Supu ikiwa tayari 

Sunday, 12 October 2014

Walimu Wa Madrsa Na Maimamu Wa Misikiti Wanatakiwa Kuwa Na Tahadhari Na Utapeli Huu.

Kuna mama mmoja wa kiarabu mwenye jina la Nuraisha Jamal Namba Ya Simu 0716 33 61 33 alipiga simu kwa mwalimu wa Madrasat Da'wat Islamiyah iliopo Kigogo Dar es Salaam kwa ustadh Hassan Ndaro kwenye namba hii 0719 11 49 55 na kumwambia ofisi yake imepokea maombi yao ya siku nyingi ya ujenzi wa Madrsa na maombi yamekubaliwa na waende Mororgoro wakachukue pesa zisizo pungua Tsh milioni 40.

Walimu wale wakajikusanya na wakaenda walimu wawili uko Morogoro na kufikia jilani na benki ya NBC mjini Morogoro .
Walipo mpigia simu yule mama akawaambia kuwa gharama za ujenzi zimepanda kwa hiyo bora waongee na mkubwa wake wa kazi ili awaongezee pesa. Akawapa namba ya simu ya huyo aliyeitwa mkubwa na wakaongea naye na akawapa ahadi ya kuwaongezea Tsh milioni 34, na akawata waende Tawa la benki NBC pamoja na nyaraka zao na wamkabidhi karani aliyewaelekeza.

Walipoingia benki na kuonana na yule karani, akawaambia kuwa nyaraka zina mapungufu. Na ili awasaidie akawataka watoe Tsh laki mbili (Rushwa), na nyaraka  zikikamilishwa zitatumwa kwa fax kwa wahusika. Yule karani akawataka wazitume zile pesa kwa Yule mama wa Kiarabu kwa kutumia tigo pesa. Kisha wakatakiwa warudi zao Dar es Salaam na kuagizwa waende benki ya NBC Magomeni siku ya Ijumaa ya tarehe 26/09/2014 na wamuone mtu mwingine mwenye namba 0789 079 539 na atawapa hela zao kutoka account namba 2017 4285 8422.
Walipokwenda kwa Yule mtu walie agizwa kwake naye akawadai rushwa ya Tsh laki mbili na wazitume kwa yule yule mama wa Kiarabu.
Wale Waalim kufikia hapo wakawa wanazungurushwauku mara kule na hawajapewa hela walizo ahidiwa na wala hawajarudishiwa pesa zao walizotoa ili kuwezesha kupata huo msaada kwa ajili ya madrasa zao.

Maelezo haya ni kwa mujibu wa Mwalimu mkuu wa Madrasat Da'awah Sheikh Ramadhani Ndaro anapatikana kwa namba hizi 0755 26 62 90.

Tukio kama hili limeikuta Madrasat Shaadhifyyah ya Ustadh Hashim mwenye namba 0783 53 74 74, iliyopo maeneo ya Buguruni kwa Makukula. Nao walitakiwa watoe laki mbili ya fax ili kufanikisha huo msada , walipokosa laki mbili huyo mama akawaambia yeye atatoa laki moja na wao watoe laki moja. Na wakipokosa na kuanza kupata wasi wasi akawaambia waende ofisini kwake Morogoro kama alivyosema mmoja wa wanafunzi ya Madrasah hiyo Bwana Suleiman Ally mwenye namba 0714 35 32 22.

Kwa Maelezo Zaidi Wasiliana Na Ustadh Musa Kileo kwa namba hii 0754 39 39 95 au kwa email hii: Kileomja@gmail.com

Friday, 3 October 2014

Assalamu Alaikum Wa Rahmatu Allah Wa Barakatuh

‘Iydul-Adhw-haa Al-Mubaarak'
Taqabbala Allaahu Minnaa Wa Minkum
Imetoka kwa Abu Qataadah (Radhiya Allaahu 'anhu) ambaye amesema: 
Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kasema: 
“Swawm ya 'Arafah nataraji (kwa Allaah) kufuta madhambi ya mwaka uliopita na wa baada yake.” 
[Muslim].




Saturday, 9 August 2014

 
Katika pitapita zangu Mitandaoni, nikiokoteza iki na kile, ghafla nikakutana na simulizi iliyovuta macho yangu, kiasi nikaona si vibaya nikaisoma na kushea na wadau, labda nao wanaweza kufaidika kwa namna moja au nyingine. Kumbuka kuwa haya ni mawazo yake mwandishi na hayana uhusiano wowote na blog ya JIko Langu. Kichwa cha bandiko ili kilikuwa:
Ndugu zangu sio kila kinachonga'aa ni dhahabu majuu sio mchezo, Nimekibadilisha na kuipa jina lingine Maisha Ughaibuni, ili kuvutia wasomaji wetu.

- Leo naomba mnipe nafasi nijaribu kuwasaidia baadhi ya ndugu zangu Wabongo ambao hawajafika Majuu na wanaota kufika huko, kwenda kutafuta maisha maana wanaamini kule ni Paradise.

Binafsi nilikuwa na hiyo ndoto nikaitimiza na kujionea mwenyewe na nikajifunza kwamba sio kila kinachong'aa ni dhahabu. I was once a believer of that theory kwamba Majuu ndio kila kitu mpaka nilipofika huko na kujionea mwenyewe kwa macho yangu baada ya kuishi huko miaka 30.

- Kwanza ukifika tu kama nilivyokwenda New York City/USA wabongo wenzako hata unaowajua wanakukimbia maana hawawezi kukusaidia, tatizo la kwanza makaratasi ya kukuwezesha kufanya kazi tena kazi ambazo kwenye maisha yako hapa bongo hukutegemea kuzifanya infact ni kwa mara ya kwanza nikaona Singa singa anafanya kazi kituo cha mafuta sikutegmea kuona hayo hata siku moja.

Huna makaratasi na huna pa kukaa kama umeenda kama nilivyokwenda mwenyewe kivyako vyako, itakuchukua miezi kama 6 ya kusota sana ndio uweze kupata ID na Card ili uweze kupata kazi angalau ya kulea wazee au matahira.

- So kwa mara ya kwanza katika maisha yako unakutana na kitu kinaitwa Kodi, au taxes maana hapa bongo tunacheza cheza tu na kodi kule ni serious ishu, panga pangua huwezi kupata mshahara unaozidi Dola 500 za kimarekani kwa wiki kati ya hizo watakukata angalau 100 za kodi so utabaki na 400 tu chumba 150 kwa wiki, nauli ka kwenda na kurudi kazini, halafu unagundua ili upate hgela extra ni lazima ufanye kazi masaaa mengi, so kwa mara ya kwanza unajifunza kuishi kazini maisha yako yanakuwa ni kazini tu,

- Wazungu wana akili sana System yao wameitengeza makusudi kwamba mtu kama wewe mbongo ukienda unaichangia Uchumi wao tu, uwezekano wa wewe kuwa tajiri kwa kufanya biashara kule haupo kabisa unless uuze madawa ya kulevya, ninasema tena uwezekano wa wewe mbongo kutajirika

Majuu ni haupo kabisa labda ujiunge na kuuza madawa ambayo haitachukua muda mrefu watakushika unajua kwa nini watakushika ni kwa sababu Polisi wa majuu wana akili sana wanajua kwamba hawawezi kuzuia kabisa kuuzwa madawa ya kulevya kwa sababu moja kubwa sana nayo ni Law Enforcement ya kuzuia drugs inaajiri karibu wananchi Millioni 2 wa taifa lao.

Sasa ukizuia madawa ina maana hawa hawatakuwa na kazi kwa hiyo wanavyojifanya wanazuia madawa ni waongo sana nalijua hili kutokana na kusoma Criminology nchini kwao, so wanachofanya ni kwamba kwa mfano Mjini New York.

Polisi wameugawa mji mzima kwa vipande vipande na kukata maeneo ya wauza drugs, wanaowajua one on one lakini hawawashiki hata siku kwa sharti moja tu kwamba wasiue au wasuze ile drugs ya kujipiga sindano, kwa hiyo any crime ikitokea kwenye lile eneo polisi wanamfuata muuza drugs mkubwa pale waliomkabidhi eneo ambaye siku zote ana wafanyakazi wengi mtaani kwa hiyo anajua nani amefanya anawaambia.

Polisi mara moja unashikwa, sasa wewe mbongo kwa vile hujui hii system unajiingaiza na kuanza kuuza drugs, mwenye eneo anakujua mara moja na kuwashitua Polisi ndio mwisho wako na Polisi wa Majuu hawana haraka wanaweza kukuwinda hata mwaka mzima nia na madhumuni yao kukamata system yako nzima na watakushika tu.

- Biashara ya halali huwezi kwa sababu kwanza huna capital ya kutosha na besides Wazungu wameshazoeshwa majina makubwa so siku zote wananunua kwenye maduka yenye majina makubwa, pili kodi ni kali sana huwezi kabisa maana kwenye kulipia kodi utashindwa tu so wabongo wengi majuu wanaojifanya kufanya biashara ninasema ni waongo sana always wana biashara nyingine kuliko wanayoionyesha.

- So huna choice ila kufanya kazi tu kama mbwa, ukitoka kazini ni kulala tu na kukaa ndani ya nyumba kuangalia TV hela huna mpaka mwisho wa wiki ukilipwa Wazungu wajanja sana wanakulipa kila mwisho wiki kusudi uweze kuzitumia hela zote by jumatatu ndivyo uchumi wao unavyosimama imara.

Wazungu wanajua kuwa hela wanazokulipa mshahara hazitoshi kwa hiyo wamekutengenezea system ya Credit Card yaani unapewa Card bila masharti magumu ukope, kufumba na kufumbua una madeni kuliko uwezo wako, hatimaye wanakufikisha mahali unakuwa unalipa madeni yako on interest tu bila kugusa deni lenyewe hasa deni linaendelea kuwa kubwa mpaka mwisho maisha yako ni madeni tu,

- Huku home ndugu na jamaa wanakuaminia kwamba sasa upo vizuri kumbe sio kabisa, kutuma hela huwezi wewe mwenyewe huna hela extra maana ile system haikupi hiyo nafasi, so Rafiki yako wa bongo akija unamkimbia maana huna hela extra ya kumsaidia unajificha mpaka usikie amekuwa sawa ndio unajitokeza na kujifanya kumjua sana na kwamba ulikuwa umesafiri, ndugu yako akija unamkimbia maana huwezi kumsaidia hatimaye unakata mawasiliano na home bongo maana huna pesa.

Pole pole unaanza kuwa kama Wazungu ukitembea unaongea mwenyewe kudadeki madeni yamekukaba mpaka shingoni, zamani ilikuwa rahisi ukizidiwa madeni unaenda Mahakamani una-file kufilisika wanakusamehe siku hizi hamna tena hiyo mpaka ulipe tu.

- Sasa unaanza kukumbuka bongo, hapa ulikuwa na kazi nzuri ulikuwa unaweza kula mara tatu kwa siku unaweza kwenda bar kunywa kidogo, unaweza kwenda uwanja wa Taifa kuona mipira mikubwa.

Majuu forget it it will never happen huwezi so huna pa kwenda matokeo yake mbongo mmoja akifanya party ya birthday hata ya mtoto mchanga wote mnakimbilia huko watuwazima unakuta mmejaa nyumbani kwa mbongo, kijumba kidogo mnabanana humo humo na kuanza kupiga picha za kutuma bongo kuwakoga wajinga kwamba upo majuu.

Pale kwenye party inatakiwa uwe very careful kwenye kupiga picha unatafuta angle ya kuonyesha upo kwenye bonge la nyumba kumbe mazishi matupu, umevaa nguo za kukopa dukani kwa credit card, kesho kazini mapema sana so hata pale kwenye party huna raha ila unajifanya kuwa furaha sana kumbe uongo mtupu madeni yamekukaba mpaka shingoni masikini wa Mungu,

- Matokeo yake unaanza kuja kwenye mitandao na kuanza kutukana Serikali ya Tanzania na Viongozi wake kisa na mkasa yamekushinda huko Majuu, na kurudi huwezi wengi wao wanaanza ku-develop tabia za ajabu na kutisha sana kisa maisha ni magumu na sivyo walivyotegemea lakini hawawezi kukubali na kusema wazi maana ni aibu.

Wazungu wametengeneza system yao ya maisha ili wanasheria na madakitari tu ndio wale bataz so wewe ukienda kule bila kusoma utachekesha tu, na uzuri wa Wazungu ni kwamba no matter what utakula tu maana kwa mfano usiku fast food zote wanatakiwa ikifika saa sita kutupa chakula kama kipo hakiruhusiwi kwenda next day kwa hiyo ukienda pale watakupa bure maana hawaruhusiwi kukitupa mpaka wahakikishe hakuna mtu anayekihitaji kwanza ni sheriaa.

- So unaanza pole pole kukumbuka bongo, furaha yako yote haipo tena Wazungu kama kawaida yao hawapendi weusi popote unapokwenda wewe ni nothing but nigga, huna thamani yoyote ni good for nothing halafu maisha majuu ni sheria asubuhi mpaka saa ya kulala!!!.........

OK GUYS KWA LEO NAOMBA NIISHIE HAPA NEXT NIKIWA NA TIME KAMA YA LEO WILL DO SOME MORE!!

Le Mutuz

Wednesday, 6 August 2014

Magadi Soda:

Magadi soda ni mazuri sana kwa kusafishia uso na haswa ukiwa na chunusi. Changanya kiasi kidogo cha magadi soda na maji ya kutosha kuunda kidonge kidogo na kisha weka au kandika kidonge icho sehemu ilio athirika na chunusi. Kwa muda wa dakika 15-20 au mpaka ikauke, na kisha suuza kwa maji yasiwe ya moto. Unaweza kurudia rudia mara kadhaa kwa siku mpaka utakapo ona athari ya chunusi imepotea.

Matango:

Unaweza kutumia Tango kwa kuondoa chunusi na hata kuondoa mabaka mabaka katika ngozi na kuifanya ngozi yako kuonekana yenye afya na yenye kuvutia.
mazuri sana kwa kusafishia uso na haswa ukiwa na chunusi. Kata tango na kasha liponde ponde (unaweza kutumia blenda) kisha paka au kandika usoni. Wacha ikae kwa muda wa dakika 15-20  kisha suuza kwa maji baridi. Unaweza kurudia kwa siku mara mbili mpaka mara tatu kwa siku.

 Kitunguu Thaumu:

Unaweza kutumia kitunguu thaumu. Kuondoa chunusi. Matumizi ya Kitunguu thaumu, uleta matokeo mazuri sana katika kuondoa chunusi usoni na hata kuuwa bacteria sababu ina kemikali (antiseptiki) inayozuia kukua kwa bakteria kwenye jeraha au ngozi iliyo athirika kwa chunusi au hata kwenye kidonda. Na pia ina viwango vya juu wa salfa (ni zuri kwa ajili kukausha mafuta kwenye ngozi ya mwili). Twanga kitungu thaumu, au unaweza kukata nusu na kubandika sehemu iliyo na chunusi shikilia kwa dakika 5-10, na kisha safisha na maji baridi. Waweza kufanya ivyo asubuhi na jioni.

Mnana (Peppermint):

Unaweza kutumia majani ya Mnanaa kuondoa chunusi usoni.
Majani ya manna utumika hata kwa wale wenye matatizo ya Mba kwenye kichwa. Twanga majani machache au saga kisha weka sehemu iliyo athirika. Wacha mpaka pakauke na kisha safisha kwa maji baridi. Unaweza kufanya hivyo mara kadhaa kwa siku.

Matumizi ya Limao:

Kata limao na kisha kwa kutumia kijiti chenye pamba kiloweke kwa maji ya limao, sugua sehemu yenye chunusi, kisha wacha pakauke, unaweza kurudia rudi kila baada ya masaa kadhaa. Usitumie maji ya limao ya kwenye chupa, kwa sababu yameweka vihifadhi kemikali zingine kiasi cha kuondoa ubora wa kemikali halisi za kwenye limao. Tumia limao alisi.

Kutumia Asali:

Matumizi ya asali ni ya asili na ufanya ngozi, iwe na afya na nyororo. Kwa sababu kwenye asali kuna virutubisho vingi vyenye kazi ya kuua vimelea (bacteria) na kuzuia uchafu na kusinyaa kwa ngozi.
Weka asali kidogo sehemu ilio athirika na iwache kwa muda mrefu kadri uwezavyo. Vilevile unaweza kupaka uso mzima au hata mwili mzima ukitaka. Sababu asali inarutubisha ngozi ya mwili na kuifanya iwe na afya na mwonekano mzuri. Ukisha ridhika na muda wa asali kwenye ngozi yako unaweza kusafisha kwa kutumia maji ya vuguvugu.

Kutumia Papai:

Unaweza kushangaa, lakini matumizi ya papai yameonyesha matokeo mazuri sana katika kuondoa chunusi usoni na kusafisha sehemu zingine za mwili.
Ponda ponda kiasi kidogo cha papai na kisha iwache kwa muda mrefu kadri uwezavyo. Ukisha ridhika na muda unaweza kusafisha kwa kutumia maji ya kawaida. Unaweza kurudia mara kadhaa kila siku kama unataka.

Dawa Ya Meno:

Unaweza kushangaa, lakini ushangazwi na matokeo mazuri ya meno yako kusafishika kwa dawa ya meno.
Kemikali zinazotumika kuuwa Bakteria wa kwenye meno, pia zina uwezo wa kupambana na bakteria wengine. Tumia dawa ya meno isiyo na gel (non-gel) paka kwenye chunusi. Ni vizuri ukatumia usiku wakati wa kwenda kulala, ila si vibaya ukipaka hata muda wa asubuhi au mchana mradi tu uwe na muda wa kutosha wa dawa kukauka ili iweze kufanyakazi vizuri.

Namna nyingine ni kuchanganya dawa ya meno na unga wa mahindi au nganoiuliosagwa na kuwa laini sana. Unaweza kupaka na kuiwacha ikauke kwa dakika tano mpaka 10.
Safisha kwa sabuni. Mchanganyiko huu unasaidia kukausha chunusi.

Matumizi ya Poda:

Unaweza kutumia baby powder kwa kupaka nyakati za usiku wakati wa kwenda kulala na na kuiwacha mpaka asubuhi.

Matumizi ya Mvuke:

Unaweza kutumia mvuke (Steam/vapour) kuondoa mafuta yaliozidi kwenye ngozi ya uso wako. Kwa kujifukisha. Kwa wale ambao hawana mashine wanaweza kujaza sufuria au bakuli kwa maji ya moto na kujifunika kwa taulo uku ukielekeza uso wao kwenye sufuria au bakuli lenye maji yanayotoa mvuke k wa dakika 5-10. Unaweza kufanya hivi pamoja na njia mojawapo nilizo zitaja hapo juu.

Tahadhari:

Njia hizi za Asili, uchukuwa muda kidogo mpaka kuona matoke ya kuridhisha.
Njia zote hizi kama hazijaleta matokeo mazuri, tafadhali muone daktari wa ngozi au nenda hospitali ilio karibu kwa uchunguzi zaidi wa ngozi yako.

Sunday, 27 July 2014

Assalamu 'Alaykum wa RahmatuLlaah wa Barakaatuh


Jumatatu In-shaa-Allah ni tarehe 1 Shawwaal 1435H (28 July 2014) na ndio Siku kuu yetu ya ‘Iydul-Fitwr.

Kwa Munaasabah huu wa furaha ya siku hii tukufu ya ‘Iyd Al-Fitwr Napenda kuchukua fursa hii kuwawasilishia salaam zetu mimi na Familia yangu za siku hii na du'aa njema kwenu wote, tukimuomba Allah (Subhaanahu Wa Ta'ala) Atutaqabalie 'amali zetu na zenu.

Wednesday, 16 July 2014

WASIOJUA kuhusu uwezo wa asali na mdalasini wanaweza wasiamini wakiambiwa kuwa vina uwezo wa kuzuia na kutibu magonjwa hatari yaliyoshindakana hata hospitalini. Asali na mdalasini zimekuwa zikitumika kama tiba tangu enzi na enzi.

FAIDA ZA ASALI NA MDALASINI KIAFYA
Asali na mdalasini bado inaendelea kutumika kama tiba katika magonjwa ya aina mbalimbali, hasa kwa baadhi ya watu wanaoamini katika tiba mbadala kuliko tiba za kisasa, na kwa kiwango kikubwa wameweza kutibu maradhi yao bila kupata athari zingine.

Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali za kisayansi, asali ina dawa asilia ya kuua vijidudu mwilini (anti- bacterial properties). Kama ukiweka asali kwenye kidonda au mahali ulipoungua na moto, utazuia maambukizi na utaponya kidonda pia.

Ulaji wa mara kwa mara wa asali na mdalasini kwa pamoja, hutoa kinga dhidi ya ugonjwa wa moyo, kwani vyakula hivi husafisha mishipa ya damu na huyeyusha mgando wa damu kwenye mishipa. Kuziba kwa mishipa huwa ndiyo chanzo cha tatizo la shinikizo la damu na magonjwa ya moyo.

Unywaji wa asali iliyochanganywa na mdalasini kwenye maji ya uvuguvugu, utasaidia kusafisha kibofu cha mkojo na hivyo kuondoa maambukizi yoyote yanayoweza kuwepo kwenye kibofu. Kwa maana nyingine, kwa kupenda kunywa mchanganyiko huo, utajiepusha na matatizo ya kuziba kwa haja ndogo na hata saratani ya kibofu kwa kukiweka kibofu chako salama kila wakati.

Aidha, unywaji wa mara kwa mara wa mchanganyiko huo, hutoa nafuu kubwa ama huweza kuponya kabisa wenye matatizo ya ugonjwa wa baridi yabisi (arthritis). Mgonjwa anywapo mchanganyiko huu, maumivu hutoweka mara moja na kumpa nafuu ya haraka.

Vilevile, unywaji wa mchanganyiko wa asali na mdalasini huimarisha kinga ya mwili na huweza kuondoa magonjwa yote ya kuambukiza kama vile mafua au flu na huondoa mwilini baadhi ya vijidudu vinavyoambukiza magonjwa mbalimbali. Ukitengeneza mchanganyiko mzito wa asali na mdalasini na kupakaa kwenye jino linalouma utapata nafuu haraka na utazuia pia kuendelea kuuma kwa jino.

Asali na mdalasini ikitumiwa kwa pamoja pia, husadia usagaji wa chakula tumboni na hivyo kuwezesha upatikanaji wa choo laini na huzuia tumbo kujaa gesi. Asali na mdalasini pia huongeza nguvu mwilini na huchangamsha ubongo na kumfanya mtu kuwa mchangamfu kazini.

Kuna tafiti nyingine zinaonesha kuwa asali na mdalasini humuwezesha mtu kupunguza uzito kirahisi na ni kinga imara dhidi ya baadhi ya saratani. Hata hivyo, inashauriwa kutegemea vyakula hivi maarufu katika kutoa kinga ya maradhi kuliko kutegemea kama tiba zaidi, kwani kwa baadhi ya magonjwa sugu haviwezi kuponya kwa haraka.

Ili kupata faida ya asali na mdalasini kama kinga, ni vizuri kuzingatia kanuni za ulaji sahihi kwa ujumla na kutumia vyakula hivi kama sehemu ya mlo wako wa kila siku sambamba na vyakula vingine sahihi, huku ukizingatia suala la kuushughulisha mwili kwa mazoezi na kazi.

Friday, 27 June 2014


Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!