Friday, 22 February 2013


katika hii picha black soup ni hiyo ya green yenye mayai hii mboga ni tamu sana,unaweza kutumia kama kitoweo cha ugali au wali.
hii mboga ni kutoka Nigeria ni tamu sana.
Recipe
Pilipili mbuzi za kijani-itategemea na ulaji wako wa pilipili
vitunguu maji vikubwa viwili
vitungu saumu kimoja
mayai-itategemea mpo wangapi katika familia yako
Nyama kilo moja/nusu itategemea na wingi wa familia yako,ya ng'ombe,mbuzi ama kondoo ni mapenzi yako
mafuta kiasi/kama utatumia oliver oil na mafuta ya mawese itakuwa vyema zaidi
chumvi kijiko cha chai kimoja

Jinsi ya kupika
chemsha mayai yako yakiiva yatoe maganda yaweke pembeni
Chemsha nyama yako ikiiva iweke pembeni
saga kwa kutumia blender pilipili mbuzi,vitunguu maji vilivyokatwakatwa na kitunguu saumu saga hadi vilainike,bandika sufuria yako jikoni weka mafuta yako ya oliver yakipata moto mimina ule mchanganyiko uliousaga uache uchemke ukiona imekuwa inzito mimina mafuta ya mawese kiasi acha yachemke hadi likibakia rojorjo weka mayani yako na nyama uliyoichemsha.
Pia unaweza kuweka na samaki mkavu kama utapenda.
enjoy pishi nitafurahi kama ukijaribu ukatupia picha katika page ya blog.





black soup ni hiyo ya green yenye mayai
black soup ni hiyo ya green yenye mayai na vipande vya nyama  hizo nyengine hazihusiani na pishi hili.

0 comments:

Post a Comment

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!