Friday 15 November 2013

Mahitaji
Ndizi bukoba/matoke kilo moja
Nyama Nusu kilo
Kitunguu maji 1 kikubwa
Kitunguu swaumu kijiko kimoja cha chai
Nyanya mbili kubwa
Karoti kubwa moja
Pilipili hoho vipande vitatu rangin tofauti tofauti
Nazi kopo moja
chumvi nusu kijiko cha chai
Pinch moja binzari ya manjano
Jinsi ya kupika
Menya ndizi na uzioshe vizuri kisha zikata vipande viwili weka katika maji.
Weka sufuria jikoni tia mafuta kidogo weka vitunguu vikaange vkilainika weka kitunguu saumu halafu weka nyanya iliyosagwa, chumvi na binzari. weka nyama iliyochemshwa koroga, maji ya nyanya yakianza kukauka weka hoho na karoti kisha weka ndizi changanya vizuri,weka tui la nazi koroga polepole hadi ichemke sasa acha kukoroga ili ndizi ziive baada ya muda kidogo weka tui zito koroga polepole halafu iache ichemke tena. ukiona ndizi zimeiva toa.
NB: ndizi hizi ni laini na chakula cha nazi usiache maji yakauke sana sababu ikishapoa inaganda.
Chakula hiki unaweza kula mchana,au usiku na ni kwa watu watatu hadi wanne.
Shukran mdau Raphia Hussein kwa pishi.

0 comments:

Post a Comment

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!