Wednesday 13 November 2013



Mahitaji

Nyama ya mbuzi (mbavu)

Mchele vikombe 2

Tangawizi vijiko 2 vya chakula

Kitunguu swaumu kijiko 1cha chakula

Mdalasini kijiko cha chai 1

Karafuu nzima kijiko cha chai 1

Iliki nzima kijiko 1cha chai

Chumvi kijiko cha chai nusu

Limau/ndimu 

Curry powder

Zafarani

Ajnamoto

Kitunguu Maji. 1 kikubwa


Jinsi ya kupika

Chemsha nyama yako weka,curry powder,limau,chumvi,tangawizi,swaumu,karafuu na mdalasini wacha ichemke hadi Maji ya kwanza yakauke,weka Maji mengine wacha nyama ichemke hadi iive.

Toa nyama weka katika tray,weka ile supu katika bakuli pembeni,

Ile nyama iweke ktk oven kwa dk kumi moto 180 hakikisha haikauki.

Bandika sufuria jikoni kaanga vitunguu maji, weka thomu na tangawizi,hiliki na abdalasini nzima kaanga, weka ajnamoto.

Wacha vichemke Kama dakika tano weka mchele ukaange halafu weka ile supu funika,

Ukishaiva weka zafarani au hata rangi ya chakula unayoipenda.

Hakikisha unaugeuza wali kabla haujaweka rangi na pia hakikisha wali hauvunjikivunjiki.


Changanya wali na zile nyama MANDI tayari


0 comments:

Post a Comment

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!