Friday 22 February 2013

Mahitaji 
Samaki mkubwa 1
Mayai 12
Chumvi kijiko cha chai 1
Pilipili mtama kijiko cha chai 1
Limau/ndimu 1
Pilipili hoho rangi tatu 3 tofauti tofauti
Kitunguu swaumu kijiko cha chai 1
Tangawizi kijiko cha chai 1
Masala nusu kijiko cha chai
Mafuta nusu chupa

Jinsi ya kupika

Mayai

Chemsha mayai 10 yakiiva yatoe ganda la juu, na utakate kati kati toa kiini cha ndani weka pembeni.

Samaki
Mchemshe samaki wako muweke viungo vyote,ila pilipili hoho hakikisha umezikata ndogo ndogo sana.
Chemsha samaki na viungo vyote hadi aive na kusiwe na maji muache samaki apoe.
Baada ya kupoamchambue mchanganye na vile viini vya mayai.
Baada ya kuchanganya weka mchanganyiko ndani ya mayai ulikataka katikati  Kama picha inavyoonyesha.
Ukimaliza bandika karai jikoni weka mafuta,piga mayai mawili pembeni chovya kijungu ndani ya mayai na uchome.









0 comments:

Post a Comment

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!