Monday, 24 September 2012

Kila mmoja wetu atakubali kuwa tukiwa watoto wadogo bado twaenda shuleni, ifikapo saa nne au saa sita kila mmoja alikuwa akijongelea 'deli' ili apate 'barafu' au 'aisikrimu' za aidha ukwaju au ubuyu.
Kwa siye ambao sehemu ya maisha yetu tumekulia mashambani, tulikuwa tukihakisha kuwa popote penye ukwaju panageuka kijia cha msimu, walao hadi msimu wa ukwaju upite, alimradi tudokoe ukwaju.

Tunapokuwa 'wakubwa' hupenda kuona baadhi ya vyakula na matunda kama vile 'ya kitoto' na hivyo kuachana navyo, pasipo kufahamu kuwa tunakosa virutubisho vingi ambavyo ni chanzo kikuu cha afya bora.

Zifuatazo basi ni faida za ukwaju ambazo zitakushawishi siku nyingine kuagiza glasi ya juisi ya ukwaju, na kama ni 'waziri wa mambo ya ndani' ya nyumba, au una fahamiana na 'waziri husika' basi agiza aendapo gulioni asiache kuchukua fungu la ukwaju wa kutosha walao wiki kama si mwezi mzima.

Faida 10 za ukwaju:

  1. Chanzo kizuri cha viuasumu mwilini 'antioxidants' ambavyo huzuia Saratani (cancer)
  2. Chanzo cha Vitamini B na C vile vile "carotentes"
  3. Hushusha joto la mwili na kuondosha homa, hasa homa ya malaria na homa ya matumbo
  4. Huulinda mwili dhidi ya mafua na kero za mafua kooni
  5. Husaidia myeyusho na mmengenyo wa chakula na kuondosha kuvimbiwa
  6. Husaidia kutibu matatizo ya nyongo (bile disorders)
  7. Husaidia kurahisisha choo (laxative)
  8. Husaidia kupunguza wingi wa lehemu (cholesterol) na hivyo kuimarisha moyo
  9. Husaidia ngozi kuwa nyororo, vile vile husaidia ngozi inayopona baada ya kuungua au yenye vidonda
  10. Husaidia kuua minyoo tumboni (kwa watoto wadogo)

0 comments:

Post a Comment

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!