Monday 13 May 2013

Mahitaji
Biringanya kubwa 1
Mafuta kiasi
Mchele nusu kilo,ila itategemea na familia yako
Nyama/kuku itategemea na unataka kupika ya kuku au nyama
Viungo vya pilau
Chumvi
vitunguu maji vikubwa viwili
kitunguu Swaumu punje nne ila itategemea na wingi wa chakula unachopika

Jinsi ya kupika
Chemsha nyama yako au kuku wako
katakata biringanya lako katika vipande vikubwa kama inavyoonekana katika picha yakaange kwa mafuta hadi utakapoona rangi imebadilika yatoe ili yachuje mafuta
Nyama yako au kuku wako akishaive muache na supu kidogo ambayo utatumia wakati wakupika pilau yako.

Kaanga vitu vyako vyote kama vile unavyoppika pilau ya kwaida weka mchele wako,nyama au kuku, na ile supu iliyobakia ongeza na maji,wacha pilau yako ichemke,ikishaiva kabisa tumbukiza biringanya zako ziweke kwa ndani yaani zifukie na pilau.hakikisha biringanya hazipondeki pondeki.

Fuatilia kwa picha hizi hapa chini

Biringanya zikicheka katika mafuta
pilau ikiwa tayari

Nawatakia pishi jema.
Usisite kuuliza swali.

0 comments:

Post a Comment

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!