Sunday 14 July 2013



Mahitaji
Maharage 1/2
Chumvi kijiko cha chai 1
Nazi kopo 1/nazi ya kawaida 1 kubwa.
Kitunguu maji 1
Kitunguu swaumu punje 2
Binzari kidogo  ya manjano

Jinsi ya kupika
Chemsha maharage yako hadi yaive ila yasihorojeke(yasipondeke) maji yakikaribia kukauka weka kitunguu maji na swaumu,chumvi acha hadi maji yakauke weka tui la nazi kidogo lile jepesi acha hadi likauke weka pembeni.
Chukua tui zito weka katika sufiria Tia binzari koroga hadi liwe zito usiachie mkono tui litakatika.
Likishakuwa zito epua acha lipoe halafu mimina juu ya yale maharage

maharage haya unaweza tumia kwa maandazi,chapati,wengine wanalia hadi wali
Nb unaweza yamimina maharage katika bakuli au sahani halafu ndio ukamimina lile tui ulilolichemsha

0 comments:

Post a Comment

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!