Tuesday 1 October 2013



Mahitaji
Ndizi matoke kilo moja
Nyanya kopo moja
Kitunguu maji kikubwa 1
Karoti kubwa 1
Kitunguu swaumu iliyosagwa kijiko kimoja cha chai
Mafuta ya kula vijiko vya chakula 2
Pilipili hoho moja
Samaki Tilapia mmoja(itategemea na wingi wa familia yako)
Spinach(ya kutosha kwa familia yako)
Chumvi kijiko cha chakula 1
Ndimu/limau
Fish seasoning

Jinsi ya kupika
mtengeneze samaki wako ,muweka katika sufuria weka limau,chumvi kidogo,na fish seasoningmbandike jikoni muache achemke na ndimu hadi maji yakauke weka pembeni.
Menya ndizi zako zisafishe vizuri,bandika sufuria jikoni weka mafuta yakianza kupata moto weka vitunguu maji,kikianza kubadilika rangi weka swaumu kuroga ili visishike vikianza kubadilika rangi weka nyanya,karoti na ndizi wacha vichemke ongeza maji kiasi yapite ndizi kidogo tia chumvi  funika,maji yakikaribia kukauka weka hoho na samaki waki funika kwa muda wa dk tano epua.

Spinach
Weka mafuta kiasi weka kitunguu kikibadilika rangi weka spinach na chumvi funika isiive sana epua tayari kwa kuliwa.

0 comments:

Post a Comment

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!