KUKU
Kuku Mzima 1
Mayai ya kupambia 6
NAMNA YA KUMPIKA
1. Mchemshe kuku mzima na chumvi mpaka uhakikishe ameiva vizuri.
2. Mtowe na muweke pembeni. Supu yake tumia katika wali kama ilivyo hapo juuu.
3. Chemsha mayai, menya na kata vipande viwili kila yai moja weka kando
VIPIMO VYA SOSI YA KUKU YA NAZI
Kitunguu 1
Nyanya iliyokatwa vipande 1
Thomu na tangawizi 1 kijiko cha supu
Garam Masala ½ kijiko cha supu
Bizari ya manjano ½ kijiko cha chai
Chumvi Kijiko kimoja cha chai
Pilipili masala ya unga ½ kijiko cha chai
Nyanya ya kopo 1 kijiko cha supu
Nazi ya unga 1 kikombe
Maji ya ukwaju ¼ kikombe cha chai
NAMNA YA KUTAYARISHA KUPIKA
1. Tia Mafuta vijiko 2 vya supu katika sufuria
2. Kaanga kitunguu maji mpaka kiwe rangi ya udongo (brown).
3. Tia thomu na tangawizi.
4. Tia nyanya nzima iliyokatwa katwa.
5. Tia garam masala, manjano, pilipili ya unga, nyanya ya kopo, kaanga vizuri.
6. Changanya kwenye sufuria na ukwaju. Iache ichemke vizuri.
7. Changanya nazi ya unga na maji vikombe viwili.
8. Mtie kuku mpike vizuri na hilo tui.
9. Mtie kwenye oveni kidogo.
Mahitaji ya mchuzi
Kabla haujaingia katika oven
Baada ya kutoka katika oven
VIPIMO VYA WALI
Mchele 3 Vikombe
Kitunguu kikubwa kiichokatwa 1
Pilipili boga nyekundu iliyokatwa 1
Mafuta ¼ Kikombe
Zaafarani 1 kijiko cha chai
(tia kwenye kikombe na maji robo roweka)
Chumvi kijiko cha chai 1
NAMNA YA KUTAYARISHA KUPIKA
1. Katika sufuria, tia mafuta, kaanga kitunguu mpaka kiwe kidogo rangu ya udongo (brown)
2. Tia pili pili boga.
3 Tia mchele, kaanga kwa muda wa dakika 3, tia zaafarani na chumvi.
4. Tia supu uliyochemshia kuku iwe imoto.
5. Pika wali katika moto mdogo hadi uive.
hapa wali umeshaiva
KUPAKUWA KATIKA SAHANI
1. Pakuwa wali kwanza katika sinia
2. Muweke kuku juu ya wali.
3. Pambia mayai
Hivi ndio wali unavyokua na hilo sosi lake.
NB:
Nilipika Spinachya kuchemsha kwa kitunguu maji na nyanya
Pia recipe inasema kuku mzima,mie mie nimetumia kuku aliyekatatwakatwa,
0 comments:
Post a Comment