Mahitaji
unga wa ngano vikombe 2
mayai 10
maji robo kikombe,
siagi vijiko 2 vya chakula. Chumvi pinch moja
Kuku/nyama/au samaki
Pilipili hoho kila rangi
Pilipili mtama
Vitunguu maji vikubwa vinne
Limau/ndimu moja
Kitunguu swaumu kijiko 1 cha chai
Tangawizi ilisagwa kijiko 1 cha chai
Mafuta ya kupikia vikombe viwili vikubwa (kwa ajili ya kuchomea)
Njegele (kama ukipenda)
Tambi nyembamba NJIA: Chukua unga wa ngano tia kwenye bakuli vunja na mayai yote 8 tia na chumvi kidogo na maji ukoroge kisha tia kwenye blender usage wakati wa kusaga tia na siagi vijiko 2,saga hadi ulainike uwe kama uji wa mikate ya maji ila huu uwe mwepesi kidogo
Baada ya hapo pika mikate ya maji membamba ila usiitie mafuta(ikiwa membamba ndio mizuri zaidi) weka pembeni
Step 2: kuku au samaki mchemshe umeweka cumvi,ndimu,pilipili mtama,swaumu,na tangawizi,akishaiva ndio unamchanganya na vegitables zote fanya km mchanganyiko wa sambusa kisha unachukua mkate wako mmoja unautia mchanyiko wako kisha unaroll.
Hakikisha unashindilia nyama yako kusiwe na nafasi hata kidogo ili isijekutoka baadae, kisha unaukata mara 3 au 2 unavyopenda size yako.
kisha unautosa kwenye yai (haya ni yale mayai mawili uliyoyaacha)unatia kwenye tambi nyembamba unachoma
Wakati wa kuchoma mafuta yawe ya moto kama ya katles.
0 comments:
Post a Comment