Sunday 13 October 2013




Mahitaji

1 kuku aliyetolewa ngozi na umkate vipande
Tangawizi kijiko kimoja cha chai
Swaumu kijiko kimoja cha chai
coriander vijiko 2 vya chakula(chopped)
Natural Yogurt vijiko viwili vya chakula
Tomato pure vijiko viwili vya chai
Vitunguu maji 4 vikatekate na uvikaange kama vya biriani
Chumvi kijiko kimoja cha chai
Mchele vikombe viwili(Basmati)
Karafuu punje mbili(black cumin seeds)
Iliki nzima punje 4(cardamom)
Mdalasini kijiti kimoja(piece of cinnamon stick)
Viazi mbatata vikubwa vinne
Maji  175mil
Mdalisini iliyosagwa kijiko kimoja cha chai
uzile iliyosagwa kijiko kimoja cha chai
Iliki iliyosagwa kijiko kimoja cha chai
Saffron powder
Samli vijiko vya chai viwili
Mafuta ya kupikia unayopenda iwe veg,sunflower au olive
Nyanya kubwa nne
masala ya kuwasha(ukipenda)
Ndimu/limau vijiko viwili vya chai

Jinsi ya kupika

1.Roweka kuku wako katika sufuria weka tangawizi,
Swaumu, Ndimu, chumvi,nyanya,tomato pure,yogurt,Mdalisini iliyosagwa,
uzile uliosagwa kijiko kimoja cha chai
Iliki iliyosagwa  na corinder,masala kama utapenda kutumia,weka kwa muda wa masaa mawili iliviungo viingie,bandika jikoni weka moto mdogo mdogo kwa muda wa dk kumi hadi 15 weka pembeni.

2.Chukua bakuli kubwa weka mchele wako,tia chumvi kidogo weka iliki nzima,karafuu na kile kijiti cha mdalasini roweka kwa muda wa dakika kumi chuja mchele wako weka pembeni.

3.Kaanga vitunguu vyako kma vile vya biriani na viazi pia vikaange weka pembeni

4.ugawanye mchele wako katika sehemu mbili,nusu ya kwanza weka juu ya lile sosi nyunyuzia saffron,halafu weka viazi na vitunguu,halafu malizia mchele uliobakia  mimina yale maji na samli,funika bandika jikoni moto mdogo mdogo kwa muda wa dakika 35 hadi 45

chakula chako kipo tayari (unaweza kuweka rangi mbili kama utapenda,na pia unaweza pambia kwa nuts)chakula hiki unaweza kukitumia kwa watu wanne hadi sita.



0 comments:

Post a Comment

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!