Mahitaji
Mchele 2Cups
Kuku Mkubwa 1
Mayai 8(itategemea na familia yako)
Mafuta lita moja/samli 1kg
Thomu kijiko cha chakula kimoja
Vitunguu maji kilo 1
Tangawizi mbichi kijiko cha chai1
Mdalasini kijiko cha chai 1
Mdalisini nzima kipande kimoja
Iliki kijiko cha chai kimoja
Binzari ya Njano kijiko cha chai nusu
Siki kijiko cha chakula kimoja
Mtindi 1/3cup(80ml)
Nyanya kopo moja
Tomato pure Vijiko vya chakula 2
Zabibu Nyeusi(option)
Chumvi kijiko cha chakula 1
Jinsi ya kutayarisha.
Chemsha kuku weka limau/ndimu chumvi,hadi aive muweke pembeni
Vitunguu maji viagwe mara mbili,ya kwanza vikaange kama vya biriani,ya pili viweke pembeni
Mdalasini,iliki na binzari changanya pamoja,saga thomu na tangawizi mbichi na nyanya pamoja.
chemsha mayai yamenye weka pembeni
Chemsha mchele usiive sana umwage maji weka pembeni
Jinsi ya kupika Sosi
Weka sufuria jikoni tia mafuta yale uliyokaangia vitunguu kiasi,halafu tia vile vitunguu ulivyoviacha vikianza kubadilika rangi kuwa brown tia viungo ulivyosaga na kutwanga,(bakisha kidogo vitunguu na viungo kidogo)tia vipande vya kuku,mtindi,siki na supu ya kuku iliyosalia katika sufuria wacha vichemke hadi libaki rojo rojo,weka mayai,epua .
Jinsi ya kupika wali
Weka sufuria jikoni weka mafuta kidogo kaanga vitunguu ulivyoviacha tia mdalisini mzima kaanga pamoja hadi vitunguu viwe brown weka ule wali ugeuze taratibu usivunjike hadi wote uingie viungo upalie moto juu,au weka katika oven moto 180c kwa dk 10.
Wali ukikauka upakue katika sahani kubwa ili vitu vyote viingie anza na wali halafu sosi lote kuku na mayai,kisha wali tena,mwisho tupia vile vitunguuu ulivyokaanga mwanzo.
NB:mie nimetumia kuku mzima bila ya kumkata,na sosi nililiweka katika oven moto 180 kwa muda wa dk kumi,lakini unweza kutumia kuku wa vipande au hata nyama ya ng'ombe,mbuzi hata kondoo.
0 comments:
Post a Comment