Saturday 11 January 2014


Mahitaji

Kabichi moja la kiasi
Tomato pure vijiko vinne vya vyakula
Chumvi nusu kijiko cha chai
Kitunguu maji kimoja kikubwa
Kitunguu swaumu nusu kijiko cha chai
Tangawizi fresh
Limau/ndimu
Binzari ya manjano robo kijiko cha chai
Nyama Nusu(itategemea na ukubwa kabichi)
Mafuta ya kupikia vijiko 4 vya chakula(mafuta yoyote unayotumia kupikia nyumbani kwako)

Jinsi ya kupika
Osha nyma yako ibadike jikoni weka chumvi iache ichemke hadi iive weka pembeni,
katakata kabichi lako
katakata vitunguu maji weka pembeni
Bandika sufuria yako jikoni weka mafuta yakipata moto weka kitunguu maji,kikianza kubadilika rangi weka swaumu ikianza kubwa brown weka binzari ya manjano wacha vichemke ili binzari iive(maana kuna watu hawapendi harufu ya binzari)kwa hiyo wacha ichemke kwa dk mbili,weka tomato pure koroga hadi uone tomato pure imekuwa rangi ya maruni weka kabichi lako likianza kulegea weka nyama wacha kwa dakika tano weka juisi ya limao tumia kipande kimoja koroga ili limau liingia katika kabichi,wacha jikoni na moton mdogo mdogo ili lisiungue,na hakikisha haliivi kulegea.
kabichi lako likiwa tayari chukua ile tangawizi fresh itwange katika kinu au crater tumia,ukimaliza chukua tangawizi kamulia ndani ya kabichi hakikisha inaingia juisi tu ya tangawizi,baada ya hapo wacha kwa dakika tatu,epua kabichi lako.

NB:sio lazima uweke nyama unaweza pika bila ya nyama
Unaweza tumia kwa ugali,wali,au kutengenezea sandwich


2 comments:

  1. Nitajaribu kupika
    sikuwahi kuwaza kupika pishi hili

    http://www.kibuasworld.com

    ReplyDelete

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!