Saturday 11 January 2014



Mahitaji
wings kilo moja
Magi/Chicken stock
Kinguu swaumu punje 6
vitungu maji 3 vikubwa
pilipili 2 (Ukitaka)
Tangawizi nzima
Pilipili hoho 3 rangi tofautitofauti
chumvi nusu kijiko cha chai
Ndimu/limau 1
Karoti mbili kubwa
Mafuta ya kula vijiko vya chakula 4

Jinsi ya kupika
Osha wings zako vizuri weka katika sufuria/bakuli kubwa weka pembeni
Chukua vitunguu maji,swaumu,hoho,karoti,tangawizi na pilipili saga pamoja,ukimaliza mimina mchanganyiko wako wote katika wings na weka yale mafuta na ndimu,na chicken stock,acha kwa muda wa saa mbili,baada ya hapo toa wings weka katika tray choma,halafu chukua lile sosi chemsha jikoni hadi maji yote yakauke weka pembeni.
Baada ya kugeuza wings zako upande wa pili ziache zikianza kuiva paka lile sosi katika wings acha kwa dakika tano toa.
Tayari kwa kuliwa kwa ugali,wali,chapati hata mkate.
usiache zikakauka sana hazitakuwa nzuri.

0 comments:

Post a Comment

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!