Saturday 11 January 2014


Mahitaji
Tilapia wawili/unaweza tumia samaki yoyote
Kinguu swaumu punje 6
vitungu maji 3 vikubwa
pilipili 2 (Ukitaka)
Tangawizi nzima
Pilipili hoho 3 rangi tofautitofauti
chumvi nusu kijiko cha chai
Ndimu/limau 1
Karoti mbili kubwa
Mafuta ya kula vijiko vya chakula 4



Jinsi ya kupika
Osha samaki wako vizuri muweke katika sufuria/bakuli kubwa weka pembeni
Chukua vitunguu maji,swaumu,hoho,karoti,tangawizi na pilipili saga pamoja,ukimaliza mimina mchanganyiko wako wote katika samaki na weka yale mafuta na ndimu,acha kwa muda wa saa mbili,baada ya hapo toa samaki choma,halafu chukua lile sosi chemsha jikoni hadi maji yote yakauke weka pembeni
Baada ya kumgeuza samaki wako upande wa pili muache akianza kuiva paka lile sosi katika samaki acha kwa dakika tano toa.
Tayari kwa kuliwa kwa ugali,wali,chapati hata mkate.
hakikisha samaki wako hakauki sana,ili uweze kupata taste yake.
Mie nilikula kwa ugali na kabichi,recipe ya kabichi inakuja.............

0 comments:

Post a Comment

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!