Saturday, 11 January 2014



Mahitaji
Kuku mmoja mkubwa mtoe ngozi,na umkate vipande 8 hadi kumi
1/2kijiko cha chai binzari ya manjano(tumeric powder)
4 kijiko cha chakula mafuta(oliver oil,or veg oil)
3/4kikombe cha maziwa ya mgando(plain yoghurt)
1 1/2 kijiko cha chakula cumin powder
11/2kijiko cha chakula coriander powder
3 vitunguu maji
2 vijiti vya mdalasini(cinnamon sticks)
6 punge za pilipili mtama(corns whole black pepper)
3 Karafuu(Cloves)
2 pilipili za kijani(gren chillies)
2 Vijiko vya tangawizi fresh
1 kijiko cha chai cha kitunguu swaumu
1/2 kijiko cha chakula cha garam masala
1 kijiko cha chai cha chumvi kwa ajili ya taste

Jinsi ya kupika
katakata vitunguu maji vyako weka pembeni,kata na pilipili za kijani mara mbili
Weka sufuria yako jikoni au non-stic pan kubwa,weka mafuta ya kula yakipata moto kiasi weka vijiti vya mdalisini,pilipili mtama na karafuu wacha zichemke kwa dakika mbili weka vitunguu maji vikibadilika rangi,weka kitunguu swaumu kiache kwa dakika mbili,weka binzari ya manjano ikaange ili kutoa harufu, halafu weka kuku wako na spice zote zilibakia na chumvi isipokuwa yoghurt na tangawizi.
pika kwa moto mdogo mdogo kwa dk tano weka yoghurt geuza ili kuzia kushika hadi uone imebadilika rangi chukua ile tangawizi ikamue yale maji ndio uweke wacha kwa dakika mbili epua.

Mahitaji ya wali mweupe
Mchele kikombe kimoja
chumvi kiasi
karafuu punje mbili
Mdalasini kijiti kimoja kidogo.

Jinsi ya kupika wali mweupe.

Osha mchele,weka ndani ya rice cooker tia chumvi,karafuu na mdalasini weka maji vikombe viwili pika cooker ikizimika wali wako umeiva(ukitaka unaweza kuweka mafuta ya kula)
Kama unatumia sufuria weka maji katika sufuria yaache yachemke weka chumvi,karafuu,na mdalasini kisha weka mchele wako,ukianza kuchemka weka moto mdogomdogo ili kuzuia usiunguze.


NB kuku huyu anaweza kutumia kwa chapati,mkate hata maandazi.

0 comments:

Post a Comment

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!