Sunday 17 June 2012

Sanaa ya kupika chakula kwa matumizi ya binadamu ni dhana kongwe katika historia ya mwanadamu. Sanaa hii inafaida na vile vile ina hasara. Ni makusudio ya makala hii kuziweka wazi faida na hasara hizo, na hatimae kutoa mapendekezo ya namna ya kupunguza hasara hizo.

Tukianza na faida; sanaa ya kupika chakula inafaida kadhaa, baadhi yake ni hizi.

  • Kwanza, kupika chakula kunasaidia kuua vijidudu vinavyoweza kuambukiza maradhi. Kwa kawaida, vyakula vibichi huwa na vijududu ambavyo vinaweza kuambukiza maradhi. Mfano wa vijidudu hivyo ni kama vile: Salmonella typhi, ambavyo husababisha ugonjwa wa homa ya matumbo (Typhoid fever); na Vibrio cholerae ambavyo husababisha ugonjwa wa kipindupindu (Cholera). Ni vyema pia hapa tukakumbuka kuwa, chakula kilichopikwa na kupoa kinaweza kuingiwa na vijidudu vyenye kuambukiza magonjwa. Kwa hiyo, chakula kilichopoa lazima kipashwe moto tena kabla ya kuliwa.
  • Pili, kupika chakula kunasaidia chakula kuwa laini na kuweza kusagwa kwaurahisi tumboni.
  • Tatu, kupika chakula kunasaidia kuongeza utamu (radha) wa chakula. Kwa hiyo, mtuanaweza kula chakula cha kutosha.
  • Nne, kwa vile kupika chakula kunaua vijidudu na vimengenyo (enzymes), chakula kilichopikwa kinaweza kukaa kwa siku kadhaa bila ya kuharibika.
  • Tano, kupika kunapunguza kiasi cha sumu inayoweza kuiwemo katika chakula hicho. Kwa kawaida baadhi ya vyakula huwa na sumu. Kwa mfano, mihogo ambayo ni michungu huwa na sumu inayoitwa cyanide. Sumu hiyo, hasa kwenye kisamvu (majani ya mti wa muhogo) hupungua kama kisamvu kitapikwa kwamuda wa kutosha.

Hata hivyo, ikumbukwe kuwa sumu nyingine hazipungui kwa kupikwa.Jambo lakufanyakwa nyumbani ni kuacha chakula hicho.

Licha ya faida hizo; sanaa ya kupika chakula inahasara zake. Hapa tutatazama hasara mbili.
Hasara ya kwanza, kupika chakula kunaweza kusababisha upotevu wa virutubisho, hasa vitamini.
Hasara ya pili, baadhi ya vyakula kama vile mafuta (fats/oils) yanayotumika kupika vyakula kwanjia ya kukaanga (flying) yanaweza kuunguana ku toa vitu ambavyo ni sumu.

Baada ya kuona baadhi ya faida hasara za kupika chakula, vyema sasa nikamilishe makala hii kwa kutoa ushauri ufuatao:

Sanaa ya kupika vyakula ina faida nyingi kuliko hasara zake. Kwa hiyo lazima tupike vyakula vyetu. hata hivyo, vyakula hasa vyenye vitamini kama vile mboga mboga tusivipike kwa muda mrefu. Vile vile, vyombo (Sifuria) vya shaba zisitumike kupikia mboga mbonga na matunda. Pia vyombo vya kupikia lazima vifunikwe; na maji yaliyotumika kupikia ni vyema ya katumika kama supu na wala yasimwagwe. Zaidi ya hayo, mafuta yaliyofunika kukaangia (flying) vyakula yasitumike tena. 

0 comments:

Post a Comment

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!