Wednesday 31 July 2013

Mahitaji
Kuku Mmoja Mlaini
Pilipili hoho rangi tofauti tofauti nusu nusu 1/2
Chumvi kijiko kimoja cha chakula
Tangawizi kijiko kimoja cha chakula
Kitunguu swaumu kijiko kimoja cha chakula
Vitunguu maji vikubwa vitatu
Limau/ndimu kubwa moja
Korianda/katmir fresh kiasi
Pilipili mbuzi ukipenda
Pilipili mtama/black pepper nusu kijiko cha chai
Tomato pure kijiko cha chakula kimoja
Mafuta ya kupikia nusu chupa

Jinsi ya kuandaa ndizi
Menya ndizi zako zikatekate kwa jinsi unavyopenda wewe zioshe kidogo zinyunyuzie chumvi kidogo,halafu bandika karai au kikangio chako mimina mafuta yaache yapate moto kiasi weka ndizi zako zikaange hadi ziive.
ziweke katika kitchen paper ili zichuje mafuta

Jinsi ya kupika kuku
Saga kitunguu swaumu,tangawizi,korianda,pilipili mtama,pilipili mbuzi(ukipenda)na juice ya ndimu au limau pamoja weka pembeni.
Katakata pilipili hoho kubwa kubwa,na vitunguu maji pia vikubwa vikubwa weka pembeni
Katakata kuku wako na muoshe vizuri muweke katika sufuri mimina ule mchanganyoiko uliousaga na uweke chumvi acha vichemke,usiweke maji.
Ukiona maji ya viungo yanakaribia kukauka weka pilipili hoho,na vitunguu maji,na ile tomato pure funika baada ya dakika tano weka zile ndizi ndani yake halafu  ziache kwa dakika tano epua tayari kwa kuliwa.


Hapa tayari kwa kuliwa.

NB unaweza kupiga ya nyama pia,yaani baada ya kuku wewe ukatumia nyama.

0 comments:

Post a Comment

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!