Thursday 8 August 2013

Mahitaji
Nyama ya kusaga nusu
Chumvi kijiko cha chai kimoja 
Pilipili mtama nusu kijiko cha chai
Hoho Tatu rangi tofauti tofauti
Mafuta nusu chupa
Mayai 10
Unga wa mkate(crumbs bread)
Manda za sambusa
Vitunguu Maji vikubwa vitatu
Swaumu nusu kijiko cha chai
Korianda kiasi
Tangawizi kijiko cha chai kimoja

Jinsi kupika

Unachukua nyama yako ya kusaga unatia spice zote unazotaka unaibandika jikoni unaicha ichemke hadi iive.
Halafu unakatakata pilipili boga za kijani njano na nyekundu unakata ndogondogo.
Unakataka vitunguu vyako Kama vile vya sambusa unaweka kando.
Unachukua mayai yako unatapiga unaweka kando.

Unaweka chuma cha chapati jikoni unakaanga mayai,unaweka nyama na vitunguu
Ukishakaanga ukitaka kuligeuza Yai ndo unatia zile pilipili boga.


 Kama inavyoonekana katika picha unatumia manda ya sambusa unaweka mbili mbili then unakunja halafu inakatakata vipande vya size.


Kisha unachukua na ule unga wa mkate mkavu.
Halafu unapiga mayai yako unachovya kidude ndani ya mayai halafu hpembeni unazungushia huo unga wa mkate kama unalizungusha hilo gurudumu isiwe Kati huku pembeni halafu unakaanga kwenye mafuta

Tayari kwa kuliwa,hapo nimetengeneza na chatine


0 comments:

Post a Comment

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!