Thursday 8 August 2013

Mahitaji
Biringa nyembamba ndefu
Kitunguu saumu ya kutwanga kijiko 1cha chai
Chumvi kijiko 1 cha chai
Binzari ya manjano kijiko 1 cha chai
Jeera powder kijiko 1 cha chai
Pilipili ya unga(masala)kijiko 1cha chai
Giligilani ya unga kijiko 1cha chai
curry powder kijiko 1 cha chai

Jinsi ya kupika

Osha biringanya zako vizuri zipasue kwa urefu mara mbili,Weka kando. 
Changanya viungo(spice) vyote kisha jaza kwenye hizo biringanyi. 
Zipange kwny sufuria kama inavyoonekana katika picha,
Weka mafuta kidogo,weka jikoni mafuta yakianza kuchemka punguza moto funika ziive kwa mvuke(steam) kisha geuza upande wa pili nao uive.
Acha dakika kumi baada hapo zitakuwa tayari kwa kuliwa.
Biringanya hizi waweza kuzitumia kwa mihogo,ugali,wali,chapati.

                Mahitaji
       Hapo ya kugeuza upande wa pili na          baada ya kugeuza.
         Baada ya kuiva tayari kwa kuliwa

Mie nilitumia kwa pilau
Nitakutakia pishi jema.

0 comments:

Post a Comment

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!