Friday 16 August 2013


               Mkate wa nyama ndani

Mahitaji
Unga wa ngano kilo moja
Nyama ya kusaga nusu kilo
Chumvi kijiko kimoja cha chai
Sukari kijiko cha chakula 1
Mayai mawili
Samli vijiko viwili vya viwili/butter
Maziwa kikombe kimoja (mag)
Hamira pakti moja
Backing powder kijiko cha chai 1
Ndimu/limau vijiko vya chakula viwili
Tangawizi kijiko cha chai 1
Kitunguu swaumu kijiko cha chai 1

Jinsi ya kupika
Chemesha nyama yako ya kusaga  weka ndimu,chumvi,tangawizi na vitunguu swaumu hadi Maji ya kauke iache ipoe.

Katika bakuli weka  unga wako tia hamira,backing powder,sukari,pinch ya chumvi
Samli au batter,yai moja,mimina maziwa kanda hadi unga wako ulainike uwe Kama unga wa buns .
Uache kwa muda wa saa moja utamuka katakata matonge makubwa kiasi sukuma duara paka butter halafu weka nyama ya kusaga halafu roll weka katika chombo cha kuokea,ukimaliza kuzifunga zote ziache kwa nusu saa.
Baada ya nusu saa zipake ute wa Yai juu halafu ingiza katika oven weka moto 180 kwa dk 20 hadi 25.

0 comments:

Post a Comment

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!