Wednesday 4 September 2013


Mahitaji
Unga wa ngano mag 2
Hamira 1
Baking powder kijiko kimoja cha chai 1
Nazi kopo moja 400mil
Iliki kijiko cha chai 1
Maziwa ya unga kijiko cha chakula 3
Sukari robo mag
Custard powder kijiko cha chakula 2
Maji 400mil
Butter 125g

Jinsi ya kutengeneza
Weka unga wako katika bakuli changanya kila kitu kanda unga wako vizuri uwe mlaini uwe unakushika kwenye mikono kiasi.
Uache uumuke kwa muda wa saa moja,katakata matonge yako makubwa kiasi sukuma ila usisukeme sana yaani yawe manene kiasi kata mara nne weka katika tray ya kuokea wacha kwa nusu saa choma.
Moto uwe 180•C kwa muda wa dk kumi 
Maandazi yatakuwa tayari
NB:unaweza kuweka ute wa Yai kabla haujachoma ili yaweze kung'aa Kama inavyoonyesha katika picha mengine nipaka ute wa Yai mengine sijapaka.

Hii ndio nazi ninayotumia,na maji pia ninapimia hicho hicho kikopo ila Kama una jug ya kupimia itakuwa vizuri pia.

0 comments:

Post a Comment

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!