Wednesday 11 September 2013




Mahitaji

Chicken Franks(Soseji)
Fresh Tomato/unaweza tumia zozote
Tangawizi kijiko cha chai 1
Coriander powder kijiko cha chai 1
Garam masala kijiko cha chai 1
Pilipili ya unga pinch 2.
Kitunguu swaumu kijiko cha chai 1
Mchele mag 2
Kitunguu Maji kikubwa 1
Mafuta kijiko cha chakula 3
Binzari ya njano pinch 3
Simba mbili/curry kijiko cha chai 1/2
Saffron kijiko cha chai 1/2
Mix veg mag 1/2
Chumvi kijiko cha chai 1
Soya sauce kijiko cha chai 1/2
Spring onions kijiko cha chakula 3
Viazi mbatata option 

Jinsi ya kupika viazi mbatata
Vimenye vioshe na vikaange viweke pembeni (kaanga Kama vile viazi vya biriani)

Jinsi ya kupika wali
Chukua mchele wako uchemshe uchuje Maji weka pembeni

Chukua franks zako zikatekate vile unavyotaka wewe.
Bandika sufuria yako jikoni Tia mafuta kaanga kitunguu Maji kikilainika kidogo weka swaumu na tangawizi kaanga hadi vikianza kubadilika rangi  tia franks zako wacha kama dk 3 weka nyanya wacha zilainike tia binzari na simba mbili/curry,garam masala, pilipili ya unga, coriander powder,changanya na weka mix veg koroga Tia saffron ,weka wali wako changanya weka na soya sauce na viazi ufunike kwa dk 5 funua weka spring onion wacha Kama dk 5.
Tayari kwa kuliwa.

0 comments:

Post a Comment

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!