Monday 16 September 2013

 Mahitaji
Mchele mag 2
Kuku mzima
Kitunguu swaumu kijiko cha chai 1
Zafarani kijiko cha chai 1
Limau kijiko cha chakula 1
Viazi mbatata vikubwa 3
Kitunguu Maji kikubwa 1
Mafuta ya kupikia nusu chupa
Karoti kubwa 1
Hoho 3 rangi tofauti tofauti
Garam masala kijiko cha chai kimoja
Chicken cube 2
Spring onion 1
Njegere robo
Soya souse 
Jinsi ya kupika

Weka viungo kwenye kuku Kitunguu swaumu,chumvi,masalo, food colour,ndimu. mchemshe kuku kidogo weka pembeni. 

Kaanga viazi vyako weka kando, pika wali ukishaiva weka safron wote hadi uwe rangi yellow,weka pembeni.

 Weka sufuria jikoni na mafuta kaanga vitunguu visibadili rangi weka kuku mkaange vizuri ila asiungue. weka hoho karoti na njegere( njegere uzichemshe kabla,ila kama ni zile za super market zile hazihitaji kuchemshwa) karoti, hoho na spring onion. weka chicken cubes mbili weka garam masala. na soya souse changanya vizuri weka kuku na viazi kisha wali changanya vizuri funika kwa dakika tano ili viungo viingie.
Baada ya dakika tano funua chakula kipo tayari kwa kuliwa. 
Furahia pishi na familia yako

Pishi toka kwa mdau Raphia Hussein 

NB:Hufurahi sana ninapopata Mapishi toka kwa wadau wangu shukran sana.

0 comments:

Post a Comment

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!