Sunday, 19 June 2016
Tuesday, 7 June 2016
Kutokana na familia yangu kuepuka sana Kula Mafuta hivyo vyakula vyetu vingi ninaepuka kutumia mafuta mengi wakati wa kupika au kutoweka Kabisa.
Hivyo nimeamua kutwist recipe ya Shruba nimeamua kufanya chukuchuku.
Usijali nitaweka inayotumia mafuta.
Mahitaji
Oats / ngano nusu kikombe
Nyama (mbavu) nusu kilo
Nyanya fresh moja
Kitunguu maji kimoja kikubwa
Kitunguu swaumu kijiko cha chakula1
Pilipili manga kijiko cha chai 1
Chumvi nusu kijiko cha chai
Viungo vya pilau kijiko cha chakula1
Unga wa ngano kijiko kimoja cha chakula
Korianda
Jinsi ya Kupika
Chemsha oats/ngano weka pembeni
Osha nyama yako weka katika sufuria chemsha ikiiva iache na supu
Saga viungo vyote pamoja weka
mimina katika nyama,weka viungo vya pilau,mag,pilipili manga,wacha vichemke kwa pamoja kwa dakika tano halafu weka ngano funika wacha ichemke wa nusu saa.
Weka unga wa ngano katika kibakuli n.a. maji mimina katika shruba wacha uchemke kwa dakika 10.
Epua tayari kwa kuliwa..
NB:Wakati wa kunywa waweza weka siki au ndimu upendavyo
Tuesday, 19 April 2016
KWA NINI NAKUSHAURI UPUNGUZE WANGA KIAFYA?
MADHARA MENGINE YA SUKARI
Thursday, 18 February 2016
Mahitaji
Unga wa ngano 250g
Butter 250g
Mayai 9
Baking powder kijiko cha chai1
kuku wa kusaga 2cups
Chumvi kijiko cha chai 1
Sukari 1/3cup
Kungu manga 1/2 kijiko cha chai(sio lazima)
Mdalasini kijiko cha chai 1
Curry powder kijiko cha chai 1
Kitunguu swaumu kijiko cha chai 1
Tangawizi kijiko cha chai 1
Chicken stock kijiko 1/2 cha chai
Pilipili mtama 1/2 kijiko cha chai
Ndimu/limau moja
Pilipili hoho 1/2 kila rangi
Jinsi ya kupika
Muoshe kuku wako vizuri as iwe na ngozi muweke viungo vyote mbandike jikoni isipokuwa usiweke pilipili hoho.
Mwache achemke na hayo Maji yakikauka muweke pembeni apoe.
Kama utakuwa haujapata kuku wa kusaga umechemsha kuku mzima basi akipoa mnyambue nyambue au msage katika blender,muweke pembeni.
Saga siagi na sukari pamoja na mayai 3,yakichanganyika weka unga na baking powder.
Ikichanganyika vizuri weka katika chombo cha kuchomea,chukua kuku wako changanya na mayai 3 mimina juu ya ule unga wako wa keki uliopo katika chombo cha kuchomea,halafu piga Yale mayai matatu yaliyobakia ya changanye na pilipili hoho miminia juu.
Weka katika oven moto 350.
Tuesday, 16 February 2016
Mahitaji
Mchele mag 2
Yai moja
Nazi kikopo kimoja
Hamira kijiko kimoja cha chakula mfuto
Sukari nusu mag
Baking powder pinch mbili
Maziwa ya maji yawe sawa na nazi.
Iliki kijiko cha chai kimoja.
unga wa ngano kijiko kimoja cha chakula.
Jinsi ya kupika.
Roweka mchele hadi ulainike.
Weka katika blender kila kitu kasoro unga wa ngano, saga hadi ulainike weka unga wa ngano saga kidogo mimina katika bakuli wacha kwa lisaa moja uumuke.
Choma vitumbua vyako,usivinyime mafutaa.
NB:unga wa ngano unasaidia kufanya kitumbua crunch
Saturday, 30 January 2016
Mahitaji:-
Viazi mbatata kg 1
Cornflour(starch) vijiko 2 chakula
Siagi vjk 2 chakula
Chumvi kijiko1 chai
Tomato ketchup vijiko 3 chakula
Tomato puree kijiko 1 chakula
Tandoor masala powder 1/2 kjk chai
Kitunguu saumu kilichosagwa 1/4 kijiko chai
Pili pili ya unga (red chili powder) 1/4 kijiko chai
Binzari ya unga( cumin powder) 1/4 kijiko chai
Manjano (turmeric) 1/8 kijikocchai
Pilipili ya kijani ilokatwa katwa ( green chilli) 1
Limao kipande
Mafuta ya kukaangia
Mkono mmoja kotmir kupambia (for garnish)
MAELEKEZO:-
1.Tia mafuta ktk frying pan au sufuria jikoni , moto uwe wa kati (mediuh heat). Kaanga chips zako
2.Epua acha zichuje mafuta katika paper towels kisha utazikaanga tena kwa mara ya pili zikauke zadi
3. Katika sufuria jikoni pasha moto siagi iyeyuke,toa sufuria jikoni kisha tia cornflour,pamoja na mahitaji yote isipokuwa limao na kotmir.
4 Rudisha sufuria jikoni na kisha changanya vitu vyote ukikoroga hadi mchanganyiko uwe mzito.
5 Punguza moto kisha tia chips zako na geuza zienee viungo vizuri
6 Epua kisha kamulia limao na nyunyiza kotmir ulizokata kata juu. Masala chips tayari kwa kula.
Kijiko cha chai (teaspoon)
Kijiko cha chakula (Tablespoon)
Thursday, 14 January 2016
KINACHO SABABISHA HARUFU MBAYA MDOMONI
NAMNA YA KUJUA KAMA UNA HARUFU MBAYA MDOMONI
NAMNA YA KUJILINDA NA HARUFU MBAYA MDOMONI (TIBA)
NAMNA YA KUJIKINGA NA KUONDOA HARUFU MBAYA MDOMONI!
KUPIGA MSWAKI
KUNYWA MAJI MENGI
MWISHO:
Saturday, 9 January 2016
Mahitaji
Ndizi Tamu 5
Kikopo kimoja cha Nazi
Chimvi pinch Mbili
Sukari kijiko cha chakula kimono
Iliki kijiko cha chai kimoja
Custard powder kijiko cha chai kimoja
Maziwa wa unga kijiko cha chakula kimoja
Maji mag moja
Jinsi ya kupika
Katakakata ndizi zako,ndizi moja toa vipande vinne panga katika sufuria,weka chumvi,sukari,iliki,mimina maji bandika bikini funika maji yakiukia weka nazi yako wacha ichemke usinifike,wacha kwa dk 3,chukua maziwa yako ya unga (nimetumia nido) weka katika kikombe,weka custard powder changanya na maji moto robo kikombe hakikisha vimelainika mimina katika ndizi wacha kwa dakika 3 epua ndizi zako tayari,
Chakula hiki ni kwa ajili ya watu watatu.
Unaweza kutumia kwa chai,uji wa Dona,sembe,bada/unga wa muhogo.
Nb: ndizi zisiwe zimeiva sanaaa kuepuka kuhorojeka wakati wa kupika.
Enjoy pishi lako.
Sunday, 6 September 2015
Mahitaji
Mchele 2 cups(inategemea na familia yako)
Chumvi nusu kijiko cha chai
Korianda vijiko vitatu vya vyakula(majani)
Soya souse vijiko viwili vya chakula
Vitunguu maji vikubwa vitano.
Kitoweo
Kuku 1/nyama kilo moja
Mahitaji
Kitunguu swaumu kijiko cha chakula kimoja
Tangawizi kijiko cha chakula 1
Paprika kijiko cha chakula 1
Pilipili mtama 1kijiko cha chai
Pilipili mbuzi iliyosagwa 1/2 cha chai(option)
Limao/ndimu 2
Jinsi ya kupika.
Osha kuku wako vizuri,weka spice zote na limao au ndimu. Wacha vichanganyike kwa nusu saa.
Chukua tray yako kubwa (Kama ile ya kuchomea cake)weka kuku wako humu oka kwa dk thelathini kakikisha hakauki.
Jinsi ya kupika wali
Kaanga vitunguu vyako Kama vile vya biriani viweke pembeni.
Roweka mchele wako kwa dk 15
Weka katika sufuria maji mag 3bandika jikoni yakichemka weka mchele na chumvi uangalie usishikane,na usiive sana(uchemshe kwa dk 5)
Toa kuku wako Ktk oven chukua wali wako kidogo weka juu yake halafu weka vitunguu na korianda,weka soya souse ,malizia wali uliobakia halafu nyunyizia soya souse yako juu ya wali.
Oka tena kwa dk 10 toa tayari kwa kuliwa.
Wednesday, 22 July 2015
Orodha ya vyakula vifuatavyo vimeelezwa kuwa na uwezo mkubwa wa kuimarisha kinga ya mwili na kupambana na maambukizi mengine kwa kuwa na kiasi kikubwa cha protini na virutubisho vingine.
SUPU YA KUKU
Supu ya kuku wa kienyeji inaelezwa kuwa na virutubisho vinavyosaidia kupunguza utokaji wa makamasi. Utapata virutubisho vingi zaidi ukitengeneza supu ya kuku kwa kuchanganya na mboga za majani. Weka chumvi kiasi kidogo katika supu hiyo.
VITUNGUU SAUMU
Vitunguu saumu vina kirutubisho aina ya ‘allicin’ ambacho kina uwezo wa kutoa kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali ya kuambukiza. Kitunguu saumu kinatoa kinga halikadhalika kinapunguza muda wa mtu kuumwa na mafua. Tumia kitunguu hicho kwa kupika kwenye chakula au kwa kutafuna punje zake.
CHAI
Chai, hasa ya kijani, (green tea) ina virutubisho vya kuimarisha kinga ya mwili. Utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na jarida moja la masuala ya virutubisho nchini Marekani (Journal of the American College of Nutrition) umeonesha kuwa watu wanaotumia chai kwa mpangilio maalum hawasumbuliwi mara kwa mara na mafua pamoja na magonjwa mengine ya kuambukiza, huwa salama na mafua au siku za kuumwa mafua hupungua kwa asilimia 36 ukilinganisha na wale wasiokuwa na kinga imara.
Hata hivyo, tahadhari inatolewa kwa watoto wa shule kutokupewa kiasi kingi cha chai kwa siku. Unywaji wa kikombe kimoja kwa siku kwa mtoto wa shule siyo mbaya. Kwa mtu mzima, asizidishe vikombe vitatu kwa siku. Ikumbukwe kuwa chai inapotumika kwa wingi kupita kiasi, huweza kusababisha pia tatizo la kukosa choo kwa muda mrefu. Kunywa kiasi kwa afya yako.
MACHUNGWA, PILIPILI KALI
Utafiti unaonesha kwamba ulaji wa vyakula vyenye Vitamin C kwa wingi kila siku husaidia kuondoa au kuzuia ugonjwa wa mafua. Miongoni mwa vyakula vyenye kiwango kikubwa cha Vitamin C ni pamoja na machungwa, mboga za majani aina ya Brokoli na pilipili kali.
Ili kupata kiasi kingi cha Vitamin C, inashauriwa machungwa yaliwe pamoja na nyama zake za ndani au kunywa juisi yake.
ASALI
Kama inavyojulikana, asali ni tiba ya matatizo mengi ya kiafya, miongoni mwa hayo ni pamoja na mafua. Asali inasaida kuondoa kikohozi na muwasho kwenye koo. Halikadhalika, asali inaweza kutumiwa na watoto wadogo kama dawa.
Watoto wanaoruhusiwa kutumia asali kama tiba ni wa umri kati ya miaka 2 hadi 5. Hawa dozi yao ni nusu kijiko kidogo cha asali, wenye umri wa miaka 6-11 wapewe kijiko kimoja kidogo na wenye umri kuanzia miaka 12 hadi 18, wapewe vijiko vidogo viwili vya asali wakati wa kulala.
MTINDI
Kutokana na kiwango kikubwa cha protini ilichonacho, Mtindi ni chakula kingine kinachofaa kuliwa na mtu mwenye mafua ili kupunduza siku za kusumbuliwa na ugonjwa kukohoa.
CHOKOLETI NYEUSI
Wataalamu wanakubaliana kuwa ulaji wa ‘chocolate’ nyeusi (dark chocolate) huimarisha kinga ya mwili, hivyo inapoliwa na mgonjwa wa mafua huweza kumpa ahueni mgonjwa kwa namna moja ama nyingine. Halikadhalika huwa kinga kwa maambukizi mengine.
PWEZA
Samaki aina ya pweza wana virutubisho vingi vya kuongeza kinga ya mwili yenye uwezo wa kupambana na bakteria pamoja na virusi vya mafua. Kiasi kidogo cha pweza, awe wa kukaangwa au kuchemshwa kama supu, anafaa kuliwa mara kwa mara kuimarisha kinga ya mwili.
VIAZI VITAMU
Kirutubisho aina ya ‘Beta-carotene’ huimarisha kinga ya mwili. Kirutubisho hicho huwa ni muhimu kwa ustawi na uimarishaji wa kinga mwilini na kinapatikana kwa wingi kwenye viazi vitamu na vyakula vingine kama vile karoti, maboga na mayai, (kiini).
Kwa ujumla, suala la kuimarisha kinga ya mwili ni muhimu kwa afya zetu. Ulaji wa vyakula vilivyotajwa hapo juu na vingine, unatakiwa kuwa ni wa mara kwa mara kama siyo wa kudumu, kwa sababu mwili unapokosa kinga imara, ni rahisi kushambuliwa na maradhi ya kuambukiza.