Friday, 22 February 2013







Mahitaji
ngogwe/nyanya chungu tano zile kubwa
nyanya fresh mbili kubwa
chumvi nusu kijiko cha chai
pilipili boga nusu,unaweza kuweka rangi tofauti tofauti
pilipili mbuzi kama ukitaka
Maji mag moja

Jinsi ya kupika
osha gongwe zako zikate katikati usizimenye
katakata pilipili boga zako weka pamoja
mimina yale maji na chumvi bandika jikoni acha vichemke ukiona maji yanakaribia kukauka kataka kata vili nyanya slice kubwa kubwa mimina funika wacha hadi maji yakauke epua.
Pishi linakuwa tayari unaweza kula kwa mkate,ugali, wali.au kula hivyo hivyo kwa wale wanaofanya diet.




katika hii picha black soup ni hiyo ya green yenye mayai hii mboga ni tamu sana,unaweza kutumia kama kitoweo cha ugali au wali.
hii mboga ni kutoka Nigeria ni tamu sana.
Recipe
Pilipili mbuzi za kijani-itategemea na ulaji wako wa pilipili
vitunguu maji vikubwa viwili
vitungu saumu kimoja
mayai-itategemea mpo wangapi katika familia yako
Nyama kilo moja/nusu itategemea na wingi wa familia yako,ya ng'ombe,mbuzi ama kondoo ni mapenzi yako
mafuta kiasi/kama utatumia oliver oil na mafuta ya mawese itakuwa vyema zaidi
chumvi kijiko cha chai kimoja

Jinsi ya kupika
chemsha mayai yako yakiiva yatoe maganda yaweke pembeni
Chemsha nyama yako ikiiva iweke pembeni
saga kwa kutumia blender pilipili mbuzi,vitunguu maji vilivyokatwakatwa na kitunguu saumu saga hadi vilainike,bandika sufuria yako jikoni weka mafuta yako ya oliver yakipata moto mimina ule mchanganyiko uliousaga uache uchemke ukiona imekuwa inzito mimina mafuta ya mawese kiasi acha yachemke hadi likibakia rojorjo weka mayani yako na nyama uliyoichemsha.
Pia unaweza kuweka na samaki mkavu kama utapenda.
enjoy pishi nitafurahi kama ukijaribu ukatupia picha katika page ya blog.





black soup ni hiyo ya green yenye mayai
black soup ni hiyo ya green yenye mayai na vipande vya nyama  hizo nyengine hazihusiani na pishi hili.


Hii kabichi ni tamu sana nilikula nyumbani kwa rafiki yangu toka Poland,nitamwambia anipe recipe halafu nitakuja kuwawekea hapa mjaribu.
Ila aliniambia hii kabichi wao wanakula kipindi cha christmass ijapokuwa siku nyengine pia inapikwa lakini katika kipindi hicho ndio mboga mahususi.
Mahitaji 
Samaki mkubwa 1
Mayai 12
Chumvi kijiko cha chai 1
Pilipili mtama kijiko cha chai 1
Limau/ndimu 1
Pilipili hoho rangi tatu 3 tofauti tofauti
Kitunguu swaumu kijiko cha chai 1
Tangawizi kijiko cha chai 1
Masala nusu kijiko cha chai
Mafuta nusu chupa

Jinsi ya kupika

Mayai

Chemsha mayai 10 yakiiva yatoe ganda la juu, na utakate kati kati toa kiini cha ndani weka pembeni.

Samaki
Mchemshe samaki wako muweke viungo vyote,ila pilipili hoho hakikisha umezikata ndogo ndogo sana.
Chemsha samaki na viungo vyote hadi aive na kusiwe na maji muache samaki apoe.
Baada ya kupoamchambue mchanganye na vile viini vya mayai.
Baada ya kuchanganya weka mchanganyiko ndani ya mayai ulikataka katikati  Kama picha inavyoonyesha.
Ukimaliza bandika karai jikoni weka mafuta,piga mayai mawili pembeni chovya kijungu ndani ya mayai na uchome.











Mahitaji


Mag mbili za unga Wa ngano

Sukari nusu kikombe kidogo.

Backing powder kipakti kimoja.

Mafuta ya kula nusu kikombe kidogo.

Yai moja

Maji mag moja/Ila unaweza tumia hata maziwa


Namna ya kupika.

Weka unga ktk bakuli 

Pasha mafuta yako moto yakipata mimina ktk unga,changaya tumia kijiko au mwiko vikichanganyika weka Yai lako changaya,weka sukari na backing powder changaya mimina maji au maziwa taratibu.

Kanda unga wako hadi uchanganyike wote hakikasha unga wako sio mgumu sana wala mlaini sana.

Ukiwa tayari uache kwa lisaa limoja utakuwa umeumuka.kata ma donge yako sukuma Ila sio sana kata halfcake zako mikato unayotaka wewe.

Bandika kikangio jikoni weka moto mdogo ili ziweze kuiva vizuri ndani.

Unaweza kutumia kwa chai,maziwa au soda



















hiki ni kinywaji kama vile unavykunywa soda,ila dafu unakunywa na nyama za ndani.
faida za dafu ni kusafisha kibofu hivi ndio nilikuwa nikiambiwa na marehemu mama yangu.
Ila nitajitahidi kutafuta faida kitaaalamu zaidi.














Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!